MAFUNZO MAALUM YA TAALUMA YA VIUATILIFU

 

Mamlaka ya udhibiti wa afya ya mimea na viuatilifu (TPHPA) kwa kushirikiana na umoja wa wanafunzi wanaosoma kilimo (TAUSA) katika chuo kikuu cha kilimo SUA waliandaa mafunzo maalum ya kitaaluma kwa wanafunzi wa  ndaki ya kilimo kuanzia tarehe 20/2 hadi tarehe 26/2/2023.Jumla ya washiriki 142 kutoka shahada za awali za Horticulture, Agronomy, Extension ,Crop production and management na Agriculture general walishiriki na kuhitimu mafunzo haya.
Mafunzo haya yaliendeshwa na timu ya wataalamu kutoka TPHPA chini ya mratibu wa mafunzo Ndugu Jumanne Rajab Musalama .Lengo kuu la mafunzo ilikua kuwajengea uwezo wanafunzi kuhusu viuatilifu na udhibiti endelevu wa visumbufu katika mazao mbalimbali hapa nchini.Mafunzo yaliendeshwa kwa theory na vitendo mashambani chini ya wataalamu wa kilimo.
Wanafunzi walifundishwa mada mbalimbali katika maeneo ya sheria ya afya ya mimea namba 4 ya mwaka 2020 na kanuni zake,tabia na makundi ya kemikali ya viuatilifu,fomyula mbalimbali za kemikali za viautilifu,mchakato wa usajili wa viuatilifu nchini,madhara ya viuatilifu katika afya ya binadamu,utaratibu wa uendeshaji wa biashara ya viuatilifu Pamoja na ukaguzi,matumizi sahihi na salama ya viuatilifu ,na vinyunyizio.Udhibiti wa magonjwa ya mimea,magugu,wadudu sumbufu na mfumo wa usajili biashara ya viuatilifu,vibali na uagizaji wa viuatilifu kutoka nje ya nchi.
Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uwezo na kuwasaidia wanafunzi kuepuka athari za kiafya zitokanazo na viuatilifu na uchafuzi wa mazingira,kutambua visumbufu mbalimbali ,elimu sahihi ya matumizi salama ya viuatilifu,utekelezaji wa sheria na kanuni Pamoja na usajili wa biashara za viuatilifu ambayo ni fursa hata baada ya kumaliza masomo.
Akifunga na kuhitimisha mafunzo hayo na kutoa vyeti kwa washiriki Mhadhiri msaidizi kutoka idara ya sayansi mimea vipando na mazao ya bustani Miss.Hekima Mliga aliwasisitiza washiriki kuchukua hatua ya kutoa elimu kwa wakulima wengi Zaidi,kuunda vikundi na kuanzisha biashara za viuatilifu baada ya kumaliza masomo yao na kuongeza maarifa Zaidi kwa kuendelea kujifunza na kufanyia kazi yale waliyofundishwa kuhusu viuatilifu na udhibiti wa visumbufu vya mazao.

TAUSA inapenda kuwashukuru uongozi wa chuo kwa kutupatia eneo la mafunzo,Rasi wa ndaki ya kilimo na mkuu wa idara kwa ushirikiano muongozo na mchango wa mali ili  kufanikisha mafunzo haya.

 

“There is a thought that poverty is a public policy failure; poverty is man-made by action and non-action: poverty can be eliminated.” ~ Benjamin Mkapa

Related Posts