Dume bora wa ng’ombe maziwa kutoka SUA ashangaza watu.

Dume bora wa mbegu wa kisasa aina ya Fresian ambaye ni kwa ajili ya kuzalisha ng’ombe bora wa maziwa anapatikana nanenane kwenye banda la Sokoine University of Agriculture kwenye kitengo cha wanyama cha idara ya Model Training Farm. Dume huyu amekua kivutio kikubwa kwa wageni wengi wanaotembelea mabanda ya SUA

Dume (Kitulo) akiwa kwenye banda lake

Dume huyu anavutia watu wengi kutokana na ukubwa wake  na umbo ambao ni tofauti na ng’ombe wengi wa kisasa waliozoeleka na uzito wake unakadiriwa kufika kilo 1000.

Wanafunzi wakiwa wamevutiwa na Dume wetu

Dume huyu mwenye jina la kitulo amekuwepo shambani kuanzia mwaka 2018 na katika kipindi chote amefanikiwa kuzalisha ndama wengi na ambao wamekua ng’ombe bora wa maziwa lakini pia kutoa madume bora mbegu pia.

Banda bora kwa ajili ya kufugia ng’ombe

Tunawakaribisha jamii ya watu wa morogoro na watu wa jirani na watanzania kwa ujumla kujifunza njia bora za ufugaji wa ng’ombe bora wa maziwa na wanayama wengine kutoka Magadu animal Farm inayopatikana kwenye Idara ya shamba la mafunzo.

Kitulo akifurahia malisho ya nyasi

 

Related Posts